MCHUNGAJI WA MIAKA 70 AFIA KWENYE NYUMBA YA MUUMINI

Screen Shot 2014-02-21 at 3.08.40 PM
Ni moja ya taarifa ambazo nimezisikia sana kwa wiki hii hapa Nairobi inayosema kuhusu Mchungaji mmoja maarufu kwenye mji huu kwa jina la Geofrey Maingi wa kanisa la Redeemed Gospel alikutwa amefariki kwenye chumba cha kulala cha mama ambae ni muumini wake huko Buruburu.
Vyombo mbalimbali vya Kenya vimeripoti kwamba kwamba marehemu aliekua na umri wa miaka 70, alikua amekwenda nyumbani kwa mama ambae ni muumini wake kwa lengo la kumfanyia maombi lakini akafariki wakati maombi yakiendelea.
Mama huyu ambae amesema ana umri wa miaka 40, amewaambia Polisi kwamba Marehemu alizirai wakati wakiwa kwenye maombi na kwamba hawakuwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi japo majirani wanasema wawili hawa walikua wapenzi.
Baadhi ya mashuhuda wanasema Mchungaji huyu amekua na kawaida ya kwenda kwenye nyumba ya huyu mama kila weekend, na mara nyingi amekua akienda Jumamosi na kuondoka Jumatatu.
Mke wa Marehemu alizimia baada ya kupata taarifa za kifo cha mume wake ambacho kimetokea wiki mbili baada ya mchungaji mwingine wa Embu kufumaniwa na mke wa mtu.


Mwili wa mchungaji ukiwa unatolewa kweye chumba alichofia.
      Mwili Wa Marehemu Ukitolewa Kutoka Sehemu Alipofia

 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family