MBASHA: NIMEMSAMEHE NA NIPO TAYARI KUISHI NAYE KAMA ATAKUJA KUNIANGUKIA MIGUUNI! UNAJUA NI NANI? SOMA HAPA
Muimbaji wa muziki wa Injili, Flora Mbasha amesema yupo tayari kurudiana na mume wake Emmanuel Mbasha, ikiwa atakwenda kumuangukia miguuni na kumuomba msamaha. Flora alisema hayo wiki iliyopita alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza kutoa ushahidi wake juu ya kesi ya ubakaji inayomkabili Mbasha ambayo inasikilizwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala. “Mbasha nimemsamehe siku nyingi na nipo tayari kuishi naye iwapo atakuja kuniangukia miguuni na kuniomba msamaha… lakini hili (ubakaji) ni suala la mahakama,” alisema. Alipoulizwa baba halali wa mtoto wake wa kike aliyejifungua hivi karibuni, alisema hawezi kulizungumzia jambo hilo hivi sasa. “Siwezi kulizungumzia nikifanya hivyo nitakuwa simtendei haki mwanangu. Siwezi kubadili mitizamo ya watu jinsi wanavyotafakari kuhusu jambo hili,” alisema. |
Labels:
Muziki
Subscribe to:
Posts (Atom)