MBASHA: NIMEMSAMEHE NA NIPO TAYARI KUISHI NAYE KAMA ATAKUJA KUNIANGUKIA MIGUUNI! UNAJUA NI NANI? SOMA HAPA

mbasha
Muimbaji wa muziki wa Injili, Flora Mbasha amesema yupo tayari kurudiana na mume wake Emmanuel Mbasha, ikiwa atakwenda kumuangukia miguuni na
kumuomba msamaha.
Flora alisema hayo wiki iliyopita alipozungumza na waandishi wa habari
baada ya kumaliza kutoa ushahidi wake juu ya kesi ya ubakaji inayomkabili Mbasha ambayo inasikilizwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala.

“Mbasha nimemsamehe siku nyingi na nipo tayari kuishi naye iwapo atakuja
kuniangukia miguuni na kuniomba msamaha… lakini hili (ubakaji) ni suala la mahakama,” alisema.

Alipoulizwa baba halali wa mtoto wake wa kike aliyejifungua hivi karibuni, alisema hawezi kulizungumzia jambo hilo hivi sasa.

“Siwezi kulizungumzia nikifanya hivyo nitakuwa simtendei haki mwanangu. Siwezi kubadili mitizamo ya watu jinsi wanavyotafakari kuhusu jambo hili,” alisema.
 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family