Diamond Akiwa Na Mpenzi Wake Penny | ||||||||
Katika ule unaoonekana kama mwendelezo wa kendo
ndani ya tasnia ya bongo movies hatimaye Jana bongomovies.com waliweza
kumpata mwanadada Penny Mungilwa, mpenzi wa diamond platnumz na kufanya
naye interview ya simu kuhusu stori zilizozagaa mitaani na kwenye
mtandao kuhusu kipenzi cha moyo wake “Diamond Platnumz” kukutwa katika
hoteli moja ya kifahari jijini Dar es salaam na mwigizaji mahiri wa
bongo movies Irene Uwoya, na haya ndo yalikuwa majibu yake.
Bongomovies.com : Mambo penny, mzima?
Penny (VJ Penny) : Mi mzima, sijui wewe?
Bongomovies.com : Mi niko poa tuu, sorry nilikuwa nashida ya kukuuliza maswali mawili matatu tuu?
Penny (VJ Penny) : Kama nitaweza kuyajibu,
Bongomovies.com : Haina shida, kuna stori
zilikuwa zimezagaa kwenye mitandao kuhusu ishu ya diamond na Irene
Uwoya, sasa nilitaka niulize na nipate comment zako kuhusu ishu hizi?
Penny (VJ Penny) : Sina comment,
Bongomovies.com : Vipi ishu hizi ni za kweli?
Penny (VJ Penny) : Asa mi nitajuaje? Mambo afanye Diamond na Irene, mi nitajuaje?
Bongomovies.com : Lakini sisi tunajua kuwa wewe
ndo mpenzi halali wa diamond, na stori kama hizi kwa namna moja au
nyingine lazima zinakuhusu, hata kama hazipo “direct” kwako?
Penny (VJ Penny) : Naomba nikwambie kitu
kimoja, wewe inabidi umtafute Irene na Diamond, mimi sina cha kukujibu,
sijui kama wamefanya sijui kama hawajafanya, “I don’t have an any idea”
(alisisitiza), mi sikuwepo so sijui cha kukujibu. Mi mwenyewe nimeona
kama ulivyoona wewe.
Bongomovies.com : Ila Diamond si mtu wako wa karibu sana, si unaweza kuwa na ukweli kuhusu hili jambo?
Penny (VJ Penny) : Mi najua tuko happy, kama
siku zote tunavyokuaga zamani, tuko kama tulivyokuwa juzi, jana leo na
kesho, I’m happy with my baby, kama amefanya au hajafanya I don’t know,
it not my business. I’m happy with my man, that’s it!!!!
Bongomovies.com : Vipi uhusiano wako na Irene Uwoya?
Penny (VJ Penny) : Simfahamu, na “she is not my friend” namuona kwenye magazeti tuu
Bongomovies.com : Okay, basi sawa,
Penny (VJ Penny) : Alright, thank you…
Source: BONGO MOVIES WEBSITE