Mwigizaji
Rose Ndauka amesema kuwa anapumzika kwenye tasnia ya filamu kwa mwaka
mmoja kwakuwa filamu za Tanzania zinafanana sana na anataka aje na kitu
kipya na tofauti.
Kwa mujibu wa gazeti la mwanaspoti Rose Ndauka amesema wazo hilo
limetokana na tatizo la kufanya kazi zinazojirudia mara kwa mara, hali
iliyomfanya aamue kujipa likizo ya muda ili kujipanga.
Hata hivyo kauli hiyo inaweza kuwa na utata muigizaji huyo ni
mjamzito kwa sasa na huenda hiyo ndio ikawa ni sababu kubwa ya yeye
kusimama kwa muda.
|