AJINYONGA SIKU MOJA KABLA YA MTIHANI WAKE WA KIDATO CHA NNE KWA KUHOFIA KUFELI

Mwanafunzi Aliyetakiwa Kuingia Kwenye Chumba Cha Mtihani Wa Taifa Kidato Cha Nne  Leo Hii Marehemu Khamis Mkundo Mkazi Wa Iringa Akiwa Ananing`inia Usiku Wa Kuamkia Leo Baada Ya Kujinyonga Kufatia Kuogopa Mtihani Iliyokua Inamkabili (Hofu)
 Mwanafunzi Aliyefahamika Kwa Jina La Khamis Mkundo Aliyekuwa Akitaraji Kufanya Mitihani Iliyoanza Siku Ya Leo Kupitia Kituo Alichokua Amejiandikisha Kilichofahamika Kwa Jina La"KRELLUU"Mjini Iringa.

Khamis Mkundo Mkazi Wa Mwangata C Katika Manispaa Ya Iringa Amejiua Kwa Kujinyonga Kwa Kutumia Kamba Kwa Kisa Kilichogundulika Kuwa Amechoshwa Kwa Kufeli Mara Kwa Mara  Mitihani Hiyo (NECTA-KIDATO CHA NNE) Ambayo Alikua Akirudia Kuifanya Mara Kadhaa Bila Mafanikio

Kupitia Barua Yake Ndefu Aliyo Andika Kijana Huyo Amesema Kuwa "Amefanya Hivyo Si Kwa Kujipendea Ila Amechukizwa Na Hatua Yake Ya Kufeli Mara Kwa Mara Hivyo Kuamua  Kuchukua Uamuzi Wa Kujiua Ili Kuepuka Na Aibu Katika Mitihani Ijayo ( Alimaanisha Inayoanza Leo ) Ambayo Anaamini Angefeli

Shemeji Wa Kijana Huyo Aliyefahamika Kwa Jina La "Aden Tagalile" Ameueleza Mtandao Huu Wa 2brothers9093 Blog Kuwa Tukio Hilo Limetokea Mida Ya Kati Ya Saa 12 Na Saa 1 Usiku Wa Kuamkia Leo Baada Ya Kuwepo Kwa Mazungumzo Ya Muda Mrefu Kutoka Kwa Kijana Huyo Kuonyesha Kuchukia Hatua Yake Ya Kuendelea Kurudia ( Kurisiti ) Mitihani Ya Kidato Cha Nne Bila Mafanikio.Alisema:-

"Sijapenda Kuona naendelea Kufeli Na Nipo Tayari Kwa Lolote Ili Kukwepa Aibu Ambayo Ipo Mbele Yangu"

Hata Hivyo Kufuatia Mazungumzo Hayo Kijana Huyo Aliungana Na Ndugu Zake Akiwemo Kaka Yake Aliyekua Akiishi Nae Kwa Kila Mmoja Kuondoka Nyumbani Hapo Kabla Ya Kijana Huyo Kukutwa Amejinyonga.

Mwenyekiti Wa Serikali Ya Mtaa Huo Wa Mwangata C "Bw. Salehe Mgimwa" Amethibitisha Kutokea Kwa Tukio Hilo Na Kuonyesha Ujumbe Ambao Kijana Huyo Ameuacha


Mwenyekiti Wa Serikali Ya Mtaa  Wa Mwangata C lilipotokea Tukio Hilo Ndugu Salehe Mgimwa Akisoma Barua Hiyo Iliyo Achwa Na Marehemu Khamis

Askari Kanzu Aliyefika Eneo La Tukio Akikagua Mwili Wa Marehemu Khamis Baada Ya Kujinyonga Akihofia Kufeli Mitihani Iliyoanza Leo Kitaifa Ya Kidato Cha Nne

Askari Kanzu Akiendelea Kukagua Mwili Wa Marehemu

Wananchi Wa Mwangata Mjini Iringa Wakiwa Nyumbani Kwa Marehemu Khamis Kondo,Mwanafunzi Aliyejinyonga Akihofia Kufeli Mitihani Ya Taifa Iliyoanza Leo Yakuhitimu Kidato Cha Nne

Mwili Wa Kijana Huo Ukitolewa Eneo La Tukio Na Kupelekwa Katika Vyumba Vya Kuhifadhiwa Maiti  Hospitali Ya Rufaa Ya Mkoa Wa Iringa

Mwili Huo Ukipakiwa Katika Gari La Polisi Tayari Kwenda Kuhifadhiwa Mahali Husika

Barua Aliyoacha Marehemu

Polisi Wakiondoka Na Mwili Wa Marehemu Eneo La Tukio


 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family