Angella Karashani Jumamosi hii
amekuwa mshiriki wa tatu kutoka Tanzania kutolewa kwenye mashindano ya
Tusker Project Fame msimu wa sita. Washiriki wengine wa Tanzania
walioanza kutoka kwenye msimu huu walikuwa ni Durbat na Tanah.
Jumamosi hii walimu wa academy wamefanya mabadiliko ya kushtukiza
ambapo washiriki hawakutakiwa kumwokoa mshiriki mwenzao na hivyo
kuwafanya Angel na Jennifer wote kwa pamoja kuondoka.
Fess ndiye mshiriki aliyepata kura nyingi na huku Phionah wa Rwanda akiokolewa na majaji.
Kuondoka kwa Angel aliyekuwa akitegemewa sana mwaka huu kunafanya
Tanzania imebakize mshiriki mmoja tu, Hisia na kuendelezea utamaduni wa
waimbaji wa Tanzania kutolewa mapema kwenye shindano hilo...Kunani?
Bongo5