Mfanyakazi wa Shirika la Utangazaji Nchini TBC, pichani,RAMADHAN GIZE ameuawa kwa kupigwa risasi
na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi usiku wa kuamkia leo katika eneo la
UBUNGO Maziwa Jijini DSM.
Tukio hilo limetokea baada ya watu hao kuvamia duka
moja katika eneo hilo la UBUNGO MAZIWA kwa lengo la kupora, ambapo mtu mmoja
aliyefahamika kwa jina la MWARAMI RAJABU amejeruhiwa kwa kupigwa risasi na watu
hao wanaosaidiwa kuwa majambazi.