Aliyekua akiiwakilisha nchi ya Kenya kwenye Shindano la Big Brother
Africa 2013, mwandada mrembo Huddah Monroe, ameamua kumshambulia kwa
madongo mazito rapper mwenye kipaji na mafanikio makubwa nchini Kenya
maarufu kwa jina la Prezzo.
|
Inasemekana mwanadada huyu aliamua kumtupia madongo rapper huyo
kutokana na rapper huyo kuweka Picha yake na mpenzi wake mpya katika
mtandao wa Iphoneogram, ndipo mwanadada Huddah kutoa maneno haya
“ Prezzo a stray dog Broke Ass, Still Living at your mom’s place”.
Kwa habari zilizozagaa ni kwamba mwanadada Huddah bado anaamini kuwa
rapper Prezzo bado ni mwanaume wake lakini kwa upande wa rapper huyo
inaonekana kama ameshaendelea na maisha mengine katika swala la mapenzi
na kuwa ni wivu tu unamsumbua Huddah. |
|