Ikiwa
ni zaidi ya mwezi mmoja baada ya jumba la Westgate Nairobi kuingia
kwenye headlines kutokana na kutekwa na magaidi kwa siku kadhaa nchini
Kenya, huko Marekani usiku wa November 4 2013 milio nane ya risasi
ilisikika kwenye jumba la biashara linaloongoza kwa ukubwa New Jersey
(Garden State Plaza mall) usiku wa saa tatu na dakika 20 November 4
2013.
Ni zaidi ya watu 400 walikua ndani ya jumba hilo lenye mkusanyiko wa maduka mbalimbali na
Ni zaidi ya watu 400 walikua ndani ya jumba hilo lenye mkusanyiko wa maduka mbalimbali na
baada ya milio hiyo ya risasi hali ta taharuki ilitanda na kila mmoja kukimbia huku na kule kwa kuhofia usalama wake. |
Polisi walipigiwa simu na muda mfupi baadae tayari walikua
wamelizingira jengo hilo na kuanza kusaka risasi zinatokea wapi kabla ya
kuja kugundua kwamba ni mtu mmoja aliepiga hizo risasi na baadae yeye
mwenyewe kukutwa amejiua. Hakuna mtu yeyote aliepoteza maisha zaidi yake na pia hakuna mtu yeyote aliejeruhiwa. |