BAHATI BUKUKU |
MSIBA mkubwa umeikumba familia ya msanii wa nyimbo za injili, Bahati
Bukuku ya baba yake mzazi Mzee Paul Bukuku kufariki dunia baada kuugua
kwa muda mrefu. Marehemu amefia nyumbani kwa Bahati maeneo ya Tabata,
jijini Dar es Salaam.
Akiongea na Mwandishi wetu, Bahati amethibitisha kifo cha baba yake
kilichotokea asubuhi ya leo, pia amewataka Watanzania kumuombea katika
kipindi hiki kigumu kwake. "Baba yangu amefariki leo baada ya kuugua kwa
muda mrefu, nawaomba Watanzania waniombee kwa kipindi hiki kigumu
kwangu," alisema Bahati.
2brothers9093 Blog Inatoa Pole Kwa Bahati Bukuku Pamoja Na Ndugu,Rafiki Wa Karibu Wa Familia Ya Paul Bukuku Na Yeyote Aliyeguswa Na Msiba Huu
Bwana Alitoa,.....Bwana Ametwaa....... Jina Lake Lihimidiwe