Abdulaziz Chende 'Dogo Janja'. Msanii chipukizi wa muziki wa Hip Hop, Abdulaziz Chende maarufu kwa jina la Dogo Janja, ametimuliwa katika kundi la Mtanashati Entertainment. Akizungumza na Mtandao huu, kiongozi wa Mtanashati Entertainment Ustaadh Juma Namusoma alisema kuwa sababu za kumtimua Dogo Janja ni utovu wa nidhamu, unywaji pombe, kutokwenda shule pamoja na uvutaji bangi. Aliongeza kuwa tayari amempatia nauli ya shilingi 90,000/= kurudi nyumbani kwao jijini Arusha alipotokea. Dogo Janja alitua kwa mbwembwe jijini Dar es Salaam kwa ndege Juni 22 mwaka jana akitokea Arusha na kujiunga na kundi hilo. Awali alikuwa katika kundi la Tip Top Connection linaloongozwa na Madee lakini ilitokea kutoelewana kati yao na kurudishwa kwao Arusha. Alipopigiwa simu na Mtandao huu, Dongo Janja alidai kuwa bado ni memba hai wa Mtanashati Entertainment. |
Baadhi ya mashabiki wa Dogo Janja wakati wakimsubiri Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Juni 22, 2012.
Dogo Janja akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitokea jijini Arusha Juni 22, 2012.
Dogo Janja akiwa kabebwa na mashabiki wake pamoja na baadhi ya wasanii wa kundi la Mtanashati Juni 22, 2012.
Janja akiwa na PNC baada ya kuwasili jijini Dar tayari kujiunga na Mtanashati Juni 22, 2012. |
Dogo Janja akiwa kwenye gari kuelekea makao makuu ya kundi la Mtanashati Entertainment Juni 22, 2012.