RAIS KIKWETE ATEMBELEA MGODI WA CHUMA WA LIGANGA, LUDEWA MKOANI NJOMBE
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akionesha kilele cha Central Liganga hill ambacho
ni mojawapo ya sehemu ambazo kampuni ya Sichuan Hongda ya China
itachimba mashapu ya chuma na kuyafua katika kiwanda kikubwa cha kufua
chuma kitakachoajiri watu 32, 000 katika eneo hilo lenye utajiri wa
chuma la Liganga wilaya ya Ludewa mkoani Njombe leo Oktoba 22, 2013.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Meneja mradi wa
Maganga Matatitu Resource Development Limited Bw. Lawrence Manyama
kuhusu mlima huo uliosheheni mashapu ya chuma alipotembelea eneo lenye
utajiri wa chuma la Liganga wilaya ya Ludewa mkoani Njombe leo Oktoba
22, 2013. Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na wawekezaji wa kampuni ya Sichuan Hongda
ya China ambao ni wawekezaji katika eneo lenye utajiri wa chuma la
Liganga wilaya ya Ludewa mkoani Njombe leo Oktoba 22, 2013. Kampuni hiyo
inatarajiwa kujenga kiwanda cha kufua chuma mapema mwakani
kitakachoajiri watu 32,000 kitakapokamilika. Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wananchi alipoowasili katika
uwanja wa mikutano wa Ludewa ambako alihutubia mkutano wa hadhara.