Uchunguzi umebaini kuwa mmoja kati ya wakuu wa kundi la kigaidi
la al-Shabab aliishi Uingereza kwa muda wa takribani mwaka moja.
Uingereza inajulikana kama makao ya kuwalea na kuwapa hifadhi wahalifu
na magaidi.
Shirika moja la habari la Uingereza limemnukulu mshirika na rafiki wa zamani wa Abdulkadir Mohamed Abdulkadir, ajulikanaye pia kama Ikrima, akisema mkuu huyo wa al Shabab aliishi Uingereza mwaka 2007. Amesema walikutana na Ikrima katika mtaa wa Eastleigh Nairobi, Kenya ambapo walikuwa wakivuta bangi na kutafuna miraa pamoja. Ameongeza kuwa Ikrima alielekea Norway mwaka 2004 kuomba hifadhi ya kisiasa na kisha kuingia Uingereza mwaka 2007. Aliondoka Uingereza muda huo na kuelekea Somalia kujiunga na al Shabab. Imearifiwa kuwa Ikrima ni afisa mwandamizi katika kitengo cha kijasusi cha al Shabab kijulikanacho kama 'Amniyat'.
Maafisa wa usalama Kenya wamenukuliwa wakisema yamkini Ikrima alihusika katika upangaji wa hujuma ya hivi karibuni katika jengo la maduka ya biashara la Westgate jijini Nairobi mwezi uliopita.