Na Waandishi Wetu
KUMEKUWA na maneno mengi juu ya uhusiano wa
kimapenzi kati ya staa mwenye vyeo vingi Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’
na mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kisha staa wa kikapu wa
NBA ya Marekani, Mtanzania Hasheem Thabeet Manka.
Kwa mara ya kwanza mwanadada huyo
amefunguka kupitia mahojiano maalum (exclusive interview) na gazeti bora
la burudani Bongo, Ijumaa Wikienda na kufichua mazito nyuma ya pazia.
Jokate ni Miss Tanzania namba 2, 2006/07.
Ana kofia nyingi kama mtangazaji wa Channel O, mwigizaji, mwanamitindo,
MC, mwanamuziki na video queen wa nyimbo za Bongo Fleva.
DAKIKA 150
Katika mahojiano hayo ya dakika 150 (saa 2 na nusu) yaliyofanyika
katika Makao Makuu ya Global Publishers, Bamaga-Mwenge jijini Dar es
Salaam, Jumamosi iliyopita, pamoja na uhusiano wake na mastaa hao,
Jokate anayependa kucheka na kuachia tabasamu pana, alifunguka mambo
mengine mengi;
Ijumaa Wikienda: Jokate kuna taarifa kuwa uliwahi kuwa na uhusiano na Hasheem Thabeet. Je, ni kweli? Jokate: Ni kweli. Nakumbuka ilikuwa baada ya Miss Tanzania 2006. Ilikuwa kitu kama 2007 au 2008. Ijumaa Wikienda: Uhusiano wenu ulidumu kwa muda gani? Jokate: Miaka miwili…mitatu (kicheko).
Ijumaa Wikienda: Ulikutana wapi na Hasheem na ilikuwaje?
Jokate: Tulikutana kwenye maonesho ya mavazi kwenye Ukumbi wa Water
Front, Stesheni jijini Dar. Mwanzoni tulisalimiana lakini hakukuwa na
chochote kwani nilikuwa nikikutana naye nacheka vile alivyo tall
(mrefu). Naye alicheka tu.
|