Habari hizo zimedai kuwa polisi pia imewahoji mawakala wa kampuni za simu ambao walitumiwa kusajili laini mpya za simu zilizotumika kumpigia marehemu na kutumika kupanga mauaji hayo. |
Arusha. Polisi wamefanikiwa kumtia mbaroni
mfanyabiashara tajiri wa madini ya Tanzanite huko Mirerani anayetajwa
kuwa ndiye aliyepanga na kukodi watu waliomuua bilionea Erasto Msuya.
Habari za uhakika kutoka ndani ya Jeshi la Polisi
zimedai kuwa mfanyabiashara huyo alikamatwa mwishoni mwa wiki na jana na
juzi alikuwa akihojiwa na makachero.
Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, mfanyabiashara huyo
ndiye aliyetoa fedha za kununulia pikipiki mbili zilizotumika katika
mpango huo na pia alitoa fedha kwa ajili ya kununua simu mpya na laini
mpya.
“Tumewakamata watu wametupa mwanga mzuri na huyo
mfanyabiashara ndiye aliyetoa fedha za kununua pikipiki na siku moja
kabla ya tukio zilihifadhiwa nyumbani kwake,” alidokeza polisi mmoja.
Habari hizo zimedai kuwa polisi pia imewahoji
mawakala wa kampuni za simu ambao walitumiwa kusajili laini mpya za simu
zilizotumika kumpigia marehemu na kutumika kupanga mauaji hayo.
Pikipiki hizo mbili, zilinunuliwa siku moja kabla
ya tukio zikahifadhiwa nyumbani kwa mfanyabiashara huyo hadi siku
iliyofuata ambapo aliwakabidhi wauaji na zote zimekamatwa.
Mahojiano kati ya mfanyabiashara huyo na Polisi
yamekuwa yakifanyika kwa siri na katika kituo cha polisi (jina tunalo)
na kwamba mambo ni mazuri.
lakini hakitatajwa jina lake.