WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO YAMLILIA MANGWEA
BW. ALBERT MANGWEHA, (Man
Ngwair)
1/06/2013.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, imepokea kwa mshituko
na masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha msanii wa muziki wa kizazi kipya
(Bongo fleva) Albert Mangwea, aliyefariki huko Afrika Kusini katika hospitali ya St. Hellen akiwa
katika shughuli za muziki, Jumanne tarehe
28 Mei, 2013.
Kifo cha Albert Mangwea ni pigo kubwa kwa fani ya
muziki hapa nchini, na pia kimataifa. Na kutokana na umahiri wake katika fani
hiyo ya muziki wa kizazi kipya hususan aina yake ya uimbaji ya “Free Style”
alikonga mioyo ya wapenzi wake hasa vijana ndani na nje ya nchi. Albert Mangwea atakumbukwa na wasanii na wapenzi
wa muziki kwa kipaji na juhudi zake za
kukuza muziki hapa nchini.
Serikali inawapa pole ndugu na jamaa wote na kuwaomba wawe na uvumilivu na subira
katika kipindi cha msiba. Wito wa Serikali kwa wasanii na wananchi kwa
ujumla ni kuendelea kumuenzi kwa yale
yote mazuri aliyoyafanya wakati wa uhai wake.
“Mwenyenzi Mungu ailaze roho ya Albert Mangwea mahala
pema peponi.”
Imetolewa na
Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara