Mh.Godbless Lema akihutubia wanafunzi waliokusanyika eneo la "freedom square" chuoni hapo. |
Kikosi cha kutuliza ghasia mkoani Arusha kililazimika kutumia Mabomu ya Machozi kuwatuliza wanafunzi waliokuwa wakishinikiza kuandamana baada ya mwanafunzi mwenzao kuuwawa kwa kuchomwa kisu na watu wasiojulikana majira ya saa nne usiku wa kuamkia leo. Tukio hilo liliamsha hisia za wanafunzi hao na kuwafanya wakusanyike kuelekea kwa mkuu wa mkoa wa Arusha kwa madai kwamba matatizo yao huwa hayafikishwi ipasavyo, hivyo wanataka kuyawasilisha wenyewe. Juhudi za uongozi wa chuo kuwatuliza wanafunzi hao zilishindikana, na ilipofika majira ya saa nne asubuhi, Mbunge wa jimbo la Arusha alifika katika eneo hilo kuwasikiliza wanafunzi hao. "Tunatoa dakika thelathini mkuu wa mkoa awe ameshafika hapa, kama hajafika ndani ya muda huo, tunaandamana wote, mimi mbele nyie nyuma mpaka ofisini kwake" alisema Mheshimiwa Lema.
Baada ya mkuu wa mkoa kufika eneo
la tukio aligoma kuzungumza na wanafunzi hao, akidai kwamba hawezi
kuongea mpaka Mh.Lema aondoke, ndipo atapanda kuzungumza na pia
alilalamika kwamba hamna kipaza sauti kwa hiyo hawez kupaza sauti yake
kuzungumza na watu wasio na nidhamu. Maneno hayo yalipandisha hasira ya
wanafunzi hao lakini walitulizwa, na kipaza sauti kikaandaliwa katika
ukumbi wa chuo maaruf kama "main cafetaria" ili mkuu huyo azungumze.
Wanafunzi walikusanyika eneo hilo
kumsikiliza lakini alivyoanza kuongea, wanafunzi walisikika wakimzomea
kwa madai kwamba ameonesha dharau. Wanafunzi walianza kuzomea na
kumrushia chupa zaa maji mkuu wa mkoa na hapo ndipo ilibidi mabomu ya
machozi yatumike kuwatuliza wanafunzi wa chuo hicho. Kwa muda wa masaa
mawili imekuwa ikisikika milio ya mabomu chuoni hapo mpaka hali ilipo
tulia kabisa.
Kwa sasa hali ni shwari chuoni hapo
ila polisi wametapakaa huku na kule wakisema wanamtafuta Mbunge wa jimbo
la Arusha kwa madai kuwa ndiye anaye chochea mgomo huo wa wanafunzi.
Mbunge huyo alikimbia kuelekea kusikojulikana na kutelekeza gari yake
chuoni hapo, ambayo polisi walilazimika kuivuta kwa "breakdown" car
kuelekea kituo cha polisi. kama inavyoonekana katika picha.
Gari ya Mh.Godbless Lema ikiochukuliwa na polisi kutoka eneo la tukio |
Polisi wakichukua gari ya mbunge wa jimbo la Arusha |