BREAKING NEWS: LUIS SUAREZ AFUNGIWA MECHI 10 KWA KOSA LA KUMNG'ATA IVANOVIC

BREAKING NEWS: LUIS SUAREZ AFUNGIWA MECHI 10 KWA KOSA LA KUMNG'ATA IVANOVIC

LUIS SUAREZ amefungiwa mechi 10 kwa kitendo chake cha kumng'ata Branislav Ivanovic.

Mshambuliaji huyo wa Liverpool ambaye haiishi vituko uwanjani jana alikiri kwamba alifanya kweli shambulio hilo. Na leo hii FA wamemaliza msimu wake kwa kumpa adhabu ya mechi 10. 

Kwa kawaida adhabu ya kitendo cha vurugu huwa ni mechi zisizodi 3 lakini wamesema kwamba adhabu hiyo haitoshi kwa Suarez ambaye amekuwa mtukutu kwa matukio ya ajabu ajabu kila mara. 

Suarez jana usiku alikataa kukubaliana na adhabu ya zaidi ya mechi 3. Lakini leo FA wameamua vinginevyo kwa bad boy Suarez na hivyo atakumbana na adhabu ya kutocheza mechi 10 za mashindano yaliyo chini ya FA. l

Mkurugenzi wa Liverpool  Ian Ayre alisema: "Sote klabu na mchezaji husika tumeshtushwa na kutopendezewa na maamuzi haya - tunasubiri sababu za kimaandishi kabla hatujatoa uamuzi wowote hapo kesho."

Suarez ana muda mpaka Ijumaa kupinga adhabu hiyo kwa kukata rufaa.
 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family