Mrembo huyu aliyejitambulisha kwa ni mwanafunzi wa chuo
kikuu kimojawapo mjini Iringa akilia baada ya kupokea kichapo kutoka
kwa mwanamke mfanyabiashara eneo la Miyomboni mjini Iringa baada ya
kuiba viatu vya mtumba na kuficha kwapani
Hapa akimpigia simu mpenzi wake ili aweze kumkomboa baada ya kutakiwa kulipa Tsh 50,000 kwa viatu pea mbili alizoiba .
—————————————————-
Tukio la mrembo huyo kupokea kichapo na kuvuliwa nguo na
kupokonywa simu yake na mikoba zaidi ya mitano pamoja na kiasi cha TSh
15,000 ambazo alikuwa amezihifadhi limetokea jumapili wiki hii
katika eneo la Miyomboni mjini Iringa.
Akielezea juu ya mkasa huo wa aina yake leo mfanyabiashara
huyo mama Masawe alisema kuwa eneo hilo amekuwa na kawaida ya
kuibiwa viatu katika duka lake la viatu vya mtumba …..
Mama huyu anadai kuwa mbali ya kukamatwa kwa mrembo huyo
bado amepata kukamata vijana zaidi ya wawili watanashati ambao
wamekuwa wakifika na kujifanya wakichagua viatu na kuishia kuiba na
kutoweka .
Binti huyo ambaye ni mwanachuo alifika dukani hapo na kuanza kuchagua viatu akijifanya ni mteja …..
Baada ya kuona muuza duka ameangalia pembeni, binti huyo
alichukua pea moja ya viatu na kuificha kwapani asijue kwamba
pembeni kulikuwa na mtu mwingine aliyekuwa akimwangalia….
Alipoaga na kutaka kuondoka ndipo timbwili la kichapo
lilipoanza kwa mrembo huyo ambae aliomba asipelekwe polisi na
asipewe adhabu kubwa kwa kuwa ana ujauzito wa miezi mitatu
tumboni.
Alisema kuwa kutokana na maombi ya mrembo huyo kupunguziwa
adhabu hakuweza kumfikisha polisi zaidi ya kumpa kichapo cha kufa
mtu na kumpokonya mali zote alizokuwa ametoka kuiba katika maduka ya
Miyomboni mjini hapa pamoja na simu yake ya kiganjani
(113)