Mwanamke mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja, hivi
karibuni alizua sekeseke la aina yake baada ya kumvaa mwanaume
anayedaiwa ni mume wake na kumshushia kichapo.
Tukio hilo la aina
yake lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Baa ya Corner iliyopo
Afrikasana, Sinza jijini Dar ambapo inadaiwa chanzo cha vurumai hilo ni
mwanaume huyo kutoonekana nyumbani.
Chanzo
chetu kilichokuwa eneo la tukio hilo kilitutonya kuwa, awali mwanamke
huyo alitinga katika kiwanja hicho cha kujidai asubuhi na mapema huku
akionekana kuangazaangaza huku na kule kabla ya kukutana na bwana wake
huyo na kuanza kuzozana.
“Yule mwanamke alipofika hapa alionekana
alikuja kishari na hata alivyokuwa akiongea na yule bwana wake
tulibashiri kutokea kwa ugomvi.
“Kweli…
haukupita muda mrefu tukaona wakianza kukunjana, mara mwanamke
akapandwa na hasira na ndipo sekeseke la aina yake likatokea,” kilidai
chanzo hicho.
Ikaelezwa
kuwa kutokana na jinsi walivyokuwa wakitifuana, wasamaria wema
waliingilia kati na kuwataka wayamalize badala ya kuwapa faida watu.
Kufuatia ushauri huo, wawili hao waliachiana na mwanamke akaanza kulia kisha akamlalia mwanaume huyo kifuani, wakabembelezana na kuondoka eneo hilo.
Kufuatia ushauri huo, wawili hao waliachiana na mwanamke akaanza kulia kisha akamlalia mwanaume huyo kifuani, wakabembelezana na kuondoka eneo hilo.