HABARI KUHUSU MWAKILISHI WA FIFA KUTEMBELEA WIZARA YA HABARI,VIJANA,UTAMADUNI NA MICHEZO


4Ofisa Maendeleo wa Kusini mwa Afrika wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Ashford Mamelodi (kushoto) akisistiza jambo jana alipotembelea wizara ya Habari ,Vijana,Utamaduni na Michezo. 5Katibu Mkuu Wizara ya Habari ,Vijana, Utamaduni na Michezo Bw.Seth Kamuhanda wa kwanza kulia akimsikiliza mwakilishi wa Fifa wa kwanza kushoto aliyekuja nchini kutatua mgogoro uliokuwepo kwenye uchaguzi wa rais wa shirikisho la mpira nchini katikati ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw.Leodgar Tenga katika ukumbi wa Wizara ya Habari jana jijini Dar es salaam. 6Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya  Michezo Wizara ya Habari, ,Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Loenard Thadeo kushoto kwake ni Mkurugenzi Wa Habari Bw.Assah Mwambene,Mkurugenzi wa Msaidizi wa Michezo Bi.Juliana Yasoda na Afisa Habari Mkuu wa Wizara Bw.Godlease Malisa wakimsikiliza Katibu Mkuu wa wizara hiyo Bw.Seth Kamuhanda hayupo kwenye picha . 7Wawakilishi wa fifa wakiwa kwenye picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Bw.Seth Kamuhanda aliyekaa Katikati na baadhi ya viongozi wa wizara na Shirikisho la mpira wa Miguu (TFF) wakiongozwa na Rais Leodgar Tenga  aliyeketi wa Kwanza Kushoto.
 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family