Mtu
mmoja aliyetambulika kwa jina la Athuman Salum Mkami, mkazi wa Kitongoji
cha Lunulo, Kijiji cha Kisemo mkoani Morogoro, amenusurika kifo baada
ya kukatwa mapanga na wafugaji.
Tukio
hilo lilitokea Machi 30, mwaka huu kijijini hapo ambapo ng’ombe
waliingia shambani kwake na kuanza kula mazao yake na alipojaribu
kuwafukuza, wenye mifugo hiyo walijitokeza na kuanza kumshambulia kwa
mapanga.
Akizungumza akiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili hivi karibuni, mzee huyo alisema: “Wafugaji
hao walinikata kwa mapanga, inauma sana kwani nilichokuwa nakifanya ni
kuwaondoa tu ng’ombe hao wasile mazao yangu lakini mwisho nimeambulia
kipigo pamoja na kuchukuliwa fedha na silaha yangu aina ya gobore.
“Nilikwenda kuripoti polisi kisha nikaenda kwenye zahanati ya kijijini kwetu ambapo baadaye nilitakiwa kupelekwa Muhimbili.”