WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba walitarajiwa kuondoka leo alfajiri kwenda Luanda, Angola kucheza mechi ya marudiano dhidi ya Recreativo de Libolo ya huko.Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Ofisa Habari wa Simba jana, Ezekiel Kamwaga,
kikosi hicho kitakuwa na msafara wa watu 25 ambapo ni wachezaji 18 na viongozi
saba. Wachezaji waliotarajiwa kuondoka alfajiri ya leo ni Juma Kaseja, Abel Dhaira, Nassor
Masoud ‘Cholo’, Amir Maftah, Koman Bili Keita, Juma Nyoso na Shomari Kapombe.
Wengine ni Salim Kinje, Ramadhani Chombo, Amri Kiemba, Haruna Moshi,
Kiggi Makasi, Abdallah Seseme, Haruni Chanongo, Mrisho Ngassa, Felix Sunzu na
Abdallah Juma. Kwa upande wa viongozi watakaoongozana na msafara huo ni
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hans Poppe na Mjumbe wa Kamati ya
Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Muhsin Balhabou.
Wengine ni Kocha Mkuu Patrick Liewig na msaidizi wake, Jamhuri Kihwelo, kocha wa
makipa James Kisaka, Daktari wa Timu, Dk Cosmas Kapinga na Mtunza Vifaa, Kessy
Rajab. Taarifa hiyo ilisema Simba itaondoka kwa
ndege ya Shirika la Kenya, saa 11:10 alfajiri na inatarajiwa kufika Luanda saa
nne asubuhi. Mechi ya Simba na Libolo imepangwa kucheza keshokutwa kwenye
Uwanja wa Calulo uliopo katika Mji wa Calulo Jimbo la Kwanza Sul (Kwanza
Kusini). Simba ina mtihani mkubwa kwani
itatakiwa kushinda kuanzia mabao 2-0 ili isonge mbele kutokana na kupoteza
mchezo wa kwanza kwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wiki mbili
zilizopita.