UNAJUA YAKUWA KUFANYA MAPENZI KUNAPUNGUZA MSONGO WA MAWAZO KWA WANAWAKE?INGIA HAPA KUJUA


UTAFITI uliofanywa na Chuo Kikuu cha   State cha jijini New York nchini Marekani
unaeleza kuwa manii ni nzuri kwa wanawake kwani huwaondolea msongo
wa mawazo.Pia, watafiti hao wamesema wanawake wanaofanya tendo la ndoa mara kwa mara bila kutumia kinga (mapenzi salama) wanakuwa na kiwango kidogo cha msongo
wa mawazo na hufanya vizuri katika vipimo vya akili.Hali hii wamesema wataalam hao kuwa inatokana na manii kuwa na kemikali ambazo humfanya mtu kuwa vizuri kihisia, huongeza upendo/unyenyekevu, huchochea mtu kupata usingizi na huwana angalau aina tatu za kemikali za
kuondoa msongo wa mawazo (anti-depressants). Utafiti huo uliofanywa kwa kuwahoji wanawake 293 kwa kufuatilia maisha yao ya kujamiana dhidi ya afya za akili zao. Manii huwa namchanganyiko wa kemikali aina ya cortisol ambayo huongeza upendo,kemikali aina ya esterone na oxytocin ambazo zote humfanya mtu kuwa vizuri
kihisia.Pia, huwa na homoni aina za ‘thyrotropinreleasing hormone’, ambayo huondoa msongo wa mawazo, melatonin ambayo huchochea usingizi na serotonin ambayo ni homoni inayoondoa msongo wa mawazo.Kutokana kuwapo kwa mchanganyiko wakemikali na homoni hizo kwenye manii Matokeo ya utafiti Matokeo muhimu ya utafiti huu ambao umechapishwa katika jarida la ‘Archives of Sexual Behaviour’ ni kwamba hata baada ya baadhi ya watafitiwa kuongeza kiwango chao cha kujamiana, wale ambao walikuwa hawatumii kinga yoyote walikuwa na kiwango kidogo cha msongo wa mawazo tofauti na wale ambao
walikuwa wakitumia kinga kama kondomu wakati wa kujamiana.
 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family