HATIMA YA SHEIKH PONDA KUJULIKANA MARCH 5

HATMA ya Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Shehe Issa Ponda na wenzake
49, itajulikana Machi 5, mwaka huu wakati Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
itakapotoa uamuzi kama wana kesi ya kujibu au la.Endapo washitakiwa watakutwa na kesi ya
kujibu watatakiwa kupanda kizimbani kuanza kujitetea na kama hawana kesi ya
kujibu wataachiwa huru. Shehe Ponda na wenzake 49 wanakabiliwa na mashitaka matano,
likiwemo la kupanga njama ya kutenda kosa, wizi wa mali zenye thamani ya Sh
milioni 59, uchochezi, kuingia kwa jinai na kujimilikisha kiwanja cha Chang’ombe
Markazi, kinachomilikiwa na Kampuni ya
AgriTanza.Awali, Wakili wa Utetezi, Juma Nassoro akitoa hoja za majumuisho mbele ya
Hakimu Victoria Nongwa, aliiomba Mahakama iwaone washitakiwa hawana
kesi ya kujibu, kwa kuwa upande wa mashitaka umeshindwa kujenga kesi na
kuthibitisha tuhuma dhidi ya washitakiwa. Alidai kuwa polisi walifungua kesi hiyo ya
jinai kwa jazba, kwa kuwa walikuwa na uwezo wa kuwashauri washitakiwa
wakafungue kesi ya mgogoro wa ardhi katika Mahakama zinazotatua migogoro
hiyo.Wakili Nassoro alidai katika mashitaka ya kupanga njama na uchochezi, hati ya
mashitaka haijaeleza washitakiwa walipanga na kushawishi kutenda kosa
gani.Aidha, alidai kuwa hakuna shahidi aliyeeleza ni jinsi gani washitakiwa
walipanga njama na kuiba mali hizo. Katika mashitaka ya kuingia kwa nguvu na
kujimilikisha kiwanja hicho, alidai kosa hilo lingethibitishwa endapo kungekuwa
hakuna mgogoro wa ardhi, lakini katika ushahidi wao wanaeleza kuwa
washitakiwa walikwenda kwa ajili ya kukomboa eneo lao, jambo linaloonesha
kulikuwa na mgogoro. Kwa upande wake, Wakili wa Serikali,Tumaini Kweka alidai wameleta ushahidi uliothibitisha, kuwa washitakiwa qqtwalipanga njama za kuingia na kujimilikisha eneo
hilo, kwa kuwa walikaa hapo kwa siku saba na kujenga Msikiti, pia wamekiri kukamatwa katika eneo la tukio. Alidai kwamba mshitakiwa Swalehe Mukadam alikiri katika maelezo ya onyo,
kuwa aliwashawishi watu kwenda kuokoa kiwanja hicho. Wakili Nassoro aliiomba Mahakama iwaone washitakiwa wana kesi ya kujibu na kuwaamuru wapande kizimbani kujitetea kwa tuhuma
zinazowakabili.
 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family