PAPA BENEDICT WA XVI AAGA RASMI

KIONGOZI Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Benedict XVI ameaga rasmi na kukiri hadharani, kwamba alikabiliwa na ‘dhoruba kali’ wakati wa miaka yake minane ya uongozi wa Kanisa Katoliki, lakini akasema alikuwa akiongozwa na Munguna kuhisi uwepo wake kila siku.

Papa huyo mwenye umri wa miaka 85, anastaafu rasmi leo – akiwa ni Papa wa kwanza kuachia madaraka tangu Papa Gregory XII aliyefanya hivyo mwaka 1415. Maelfu ya mahujaji jana walikusanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Peter, Vatican kumsikiliza Papa.

Mrithi wake atachaguliwa katika mkutano wa makadinali mwezi ujao. Papa Benedict aliuambia umati uliokusanyika katika makazi yake, kwamba kwake upapa ulikuwa “mzigo mzito” lakini aliukubali kwa sababu alikuwa na uhakika kwamba Mungu atamwongoza.

Kuna wakati alihisi “kama Mtakatifu Peter na mitume wake katika Ziwa la Galilaya”, alisema, akirejea hadithi ya Biblia pale wanafunzi walipokuwa wakikabiliana na mawimbi mazito na Yesu Kristo akawatokea. Kanisa hilo limegubikwa na kashfa za udhalilishaji wa kijinsia ukifanywa na baadhi ya mapadri na kuvuja kwa nyaraka za siri zikionesha kuwapo rushwa na mizozo ndani ya Vatican.

Hakujawahi kutokea Papa kuomba mabilioni ya Wakatoliki duniani kote wamwombee “na wafanye hivyo pia kwa Papa mpya”, kama Benedict XVI alivyofanya jijini Vatican jana.

Hakika jana Papa Benedict alionekana kusawajika – dhaifu, hata alipokuwa akitoa sala yake ya ufunguzi, huku akiwa amezungukwa na walinzi wa kiswisi ambao wataondolewa karibu naye leo jioni wakati atakapokuwa anauvua rasmi upapa.

Lakini uamuzi wake wa kujiuzulu unaacha nyuma changamoto kubwa za kipapa juu ya udhalilishaji wa kijinsia na kashfa za kifedha, ingawa wafuasi wake wanadai alifanya mengi kukabiliana nayo huku akikiri kuwapo kazi kubwa inayotakiwa kufanywa.

Papa aliwashukuru waumini wake kwa kuheshimu uamuzi wake wa kujiuzulu na kusema anafanya hivyo kwa ajili ya mema ya Kanisa.

“Nilichukua hatua hii (kujiuzulu) nikijua kabisa uzito wake na kwamba haikuwa kawaida, lakini kwa roho safi,” alisema katika hotuba yake. Kutokana na tangazo lake hilo la kushitua, hivi sasa Kanisa limerekebisha sheria zake ili kuruhusu kuanza mchakato wa kupata mrithi wake.

Baraza la siri la makadinali linalomchagua Papa linaloanza vikao vyake katikati ya mwezi ujao, litakuwa limebakiza muda mfupi wa kupata Papa mpya atakayesimikwa katika kipindi hiki maalumu kuliko vingine katika kalenda ya kikatoliki, Wiki Takatifu, kuelekea Pasaka, ambayo inaanza Machi 24.

Habari zinasema leo Papa atasafiri kwa helikopta kwenda katika makazi yake ya wakati wa kiangazi ya kasri la Gandolfo umbali wa kilometa 24 Kusini Mashariki mwa Roma. Ataacha rasmi upapa saa 2 usiku.

“Kwa upande mmoja, nilihisi kwamba kwa kuwa uamuzi wake wa kuacha madaraka tayari umeshafahamika, Papa Benedict amefarijika,” alisema Mkuu wa Mkutano wa Maaskofu wa Ujerumani, Askofu Mkuu Robert Zollitsch.

“Lakini pia hivi sasa anahisi huruma ya watu kwake na hivyo atakuwa mwenye huzuni na hamu ya kurudi nyumbani.”

Jana alitarajiwa kutumia muda wake wa mwisho katika makazi yake ya Vatican akiagana na makadinali ambao wamekuwa wasaidizi wake wa karibu katika kipindi chote cha miaka minane ya upapa.

Nyaraka zake binafsi zitafungwa na itakapotimia saa 2 usiku leo, walinzi wake wa kiswisi watakaokuwa katika makazi yake ya Gandolfo wataondolewa na nafasi zao kuchukuliwa na polisi wa Vatican.

Hiyo ndiyo itakuwa ishara ya mwisho rasmi wa upapa wake na mwanzo wa kipindi cha mpito cha kumpata mrithi wake. Uchaguzi papa mpya Kuanzia Machi 4, makadinali watakutana kujadili matatizo yanayolikabili Kanisa na kupanga tarehe ya kuanza uchaguzi wa siri, au Baraza la kumchagua Papa, ili kumpata mrithi wa Papa Benedict wa XVI.

Mrithi huyo atachaguliwa na makadinali 115 (wenye umri wa chini ya miaka 80) kwa njia ya sanduku la kura katika Kanisa dogo la Sistine, Vatican. Zaidi ya theluthi mbili za kura ndizo zinahitajika kumchagua papa.

Makadinali 67 waliteuliwa na Benedict XVI na waliosalia waliteuliwa na aliyemtangulia, Papa Yohanne Paul II. Karibu nusu ya makadinali hao (60) wanatoka Ulaya – 21 ni Wataliano - na wengi walishafanya kazi katika chombo cha utawala cha

 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family