Makamu
Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya TASAF Taifa Abbas Kandoro akikagua
mradi wa Mashine ya kukoboa na kusaga nafaka wa Wazee katika Mtaa wa
Mbulani kata ya Ruvuma Mjini Songea ambao wamewezeshwa kiasi cha
shilingi Milioni 8 na TASAF ikiwa ni juhudi za kukabiliana na umasikini
kwa wazee.
Makamu
mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya TASAF Taifa Abbas Kandoro akizungumza
na Wazee wa Mtaa wa Mbulani katika kata ya Ruvuma Mjini Songea mara
baada ya kukagua mradi wa Mashine ya kusaga na kukoboa nafasi wa wazee
hao
Wazee
waliopatiwa mradi wa kukoboa na kusaga nafaka katika kata ya Ruvuma
Mjini Songea wakifuatilia hotuba ya Makamu Mwenyekiti wa Kamati Tendaji
ya TASAF Taifa Abbas Kandoro kuhusu nia ya TASAF kuwezesha jamii.
Wazee
wa Kata ya Ruvuma wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati
Tendaji ya Kitaifa ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF
Wajumbe
wa kamati Tendaji ya TASAF Kitaifa wakikagua mradi wa ufugaji wa Ngombe
wa Vijana wa Mtaa wa Muungano Mjini Songea. Katika mradi huu TASAF
imewawezesha vijana kupata shilingi milioni 5 za kununulia mitamba kwa
ajili ya mradi huo
Meneja
rasilimali watu wa TASAF Tekla Makundi akichangia ushauri kuhusu
uendeshaji wa mradi wa ng'ombe wa Maziwa hasa baada ya wanakikundi cha
vijana cha Muungano Mjini Songea kudai wanakabiliwa na uhaba wa dume la
kupandishia mitamba yao
Vyumba
viwili vya madarasa vilivyojengwa katika Shule ya sekondari ya Ndongosi
Songea Vijijini vikiwa vimekamilika. Ujenzi wa vyumba hivi umechangiwa
na TASAF kwa shilingi milioni 45 na wananchi shilingi milioni 4 wakati
wa utekelezaji wa awamu ya pili ya TASAF
Makamu
Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya TASAF Taifa Abbas Kandoro akisoma nembo
ya TASAF katika jengo la vyumba viwili vya madarasa lililojengwa katika
shule ya Sekondari Ndongosi Songea Vijijini. vyumba hivyo pia vimekewa
meza na viti kwa ajili ya wanafunzi 70 pamoja na meza na makabati
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu anayeshughulikia TAMISEMI Zuberi
Tamasaba akizungumza na wanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya
sekondari ya Ndongosi Songea Vijijini