Nuru
the light ni Miongoni mwa wasanii wa Tanzania ambao wanaoishi nje ya
nchi ingawa pia Bongo ndiyo home,ana wiki kadhaa tangu arejee tena
Bongona alifunguka kitu gani kipya
kutoka kwake alichonacho hivi sasa.
Upande wa kipya kutoka kwake kwa sasa Nuru amesema anahitaji
kuwasaidia wakina mama wanaoishi peke yao yaani ambao pengine
wametelekezwa na waume wao au waliofiwa na wanahitaji mitaji kidogo ya
biashara ili kujikwamua.
Hajataja ukomo wa wanawake wangapi anaohitaji kuwasaidia lakini
anachoangalia ni wale wenye mahitaji muhimu kwa ajili ya kujiendeleza
kibiashara hasa waliokwama kipesa>>’Nataka kuwasaidia wanawake
ambao wako kwenye hali ya chini sana’
‘Natafuta wanawake na wakiona hii interview kutoka hapa waniandikie barua pepe[email] wanitumie kile ambacho
wanahitaji mimi nitawasaidia kipesa,kama mtu ana idea ya Mama Ntilie
lakini hana pesa,labda yuko tayari kuuza mchicha lakini hana pesa nipo
tayari kumsaidia au mtu ana-mgahawa anahitaji hela ndogo tu labda ya
pango’
|
‘Kuna
mtu anahitaji msaada kidogo tu kuna mtu anahitaji elfu thelathini,kuna
mtu anahitaji elfu hamsini,kuna mtu anahitaji milioni na si lazima uwe
tajiri ndo uweze kuwasaidia watu,naona mwaka huu ndio nimejiweka vizuri
kuwasaidia wenzangu’.
Zitumie dakika hizi chache kumtazama Nuru akielezea.
|