Kama
utakumbuka wiki mbili zilizopita mwanasoka bora wa dunia Cristiano
Ronaldo alitolewa nje kwa kadi nyekundu kutokana na kujihusisha na
vitendo visivyo vya kiunamichezo katika mchezo wa ligi kuu ya Spain
dhidi ya Atletico Bilbao, matokeo ya kitendo kile mchezaji huyo
alifungiwa mechi 3 za ligi.
Klabu yake ya Real Madrid walikataa rufaa kwenye chama cha soka
na rufaa yao ikatupwa, baada ya hapo Madrid wakakata rufaa tena kwenye
mahakama ya michezo nchini humo, na leo hii mapema mchana mahakama hiyo
ya michezo imetoa uamuzi wake kwamba Ronaldo alistahili adhabu yake
hivyo ataendelea kuitumikia.
Kwa maana hiyo mchezaji huyo ataukosa mchezo wa leo dhidi ya
Elche, huu ndio utakuwa mchezo wa mwisho katika kutumikia adhabu kwa
Ronaldo.