Katibu
Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Ndugu Job Masima kulia
akimkabidhi funguo ya gari Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya
kama ishara ya makabidhiano ya gari mbili pamoja na michango mingine
itakayotumika katika viteule vya jeshi vya Mkoani Rukwa.
Katibu
Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Ndugu Job Masima kulia
akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya kukagua
gari aina ya Ashok Leyland iliyotolewa na Wizara yake kwa ajili
kuimarisha viteule vya kijeshi vilivyopo Mkoani Rukwa. Katika
kukabiliana na changamoto zilizokuwa zinavikabili vitua hivyo Wizara ya
ulinzi kupitia kwa Katibu Mkuu huyo imetoa gari, boti na fedha kwa ajili
ya kuboresha makazi na miundombinu katika viteule hivyo. Kwa upande
mwingine amesema kuwa baadhi ya vifaa vingine vitatoka makao makuu ya
jeshi katika kuboresha viteule hivyo.
|
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiwasha gari hilo kama ishara
ya kupokea misaada hiyo kwa viteule vya Jeshi vilivyopo Mkoani Rukwa.
Katibu
Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Ndugu Job Masima wa
pili kushoto akitoa majumuisho ya ziara yake kwa uongozi wa Mkoa wa
Rukwa leo.
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Symthies Pangisa kushoto akizungumza
katika kikao hicho cha majumuisho ambapo amemshukuru Katibu Mkuu wa
Wizara ya Ulinzi na msafara wake kwa kazi nzuri waliyoifanya Mkoani
Rukwa katika kipindi chote cha ziara yake ya siku tatu.
Baadhi
ya wajumbe walioshiriki kikao hicho cha majumuisho wakifuatilia kwa
makini.(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa
@Rukwareview.blogspot.com)