Naam,
yumkini hotuba ya JK jioni ya leo ikawa ya kihistoria. Kwa nafasi yake,
hekima, busara na uwezo wa ushawishi alio nao, njia ya JK
atakayoionyesha leo itafuatwa na Wabunge wengi wa chama chake, na hivyo,
kumsaidia Rais na Mwenyekiti wao kutimiza azma yake ya kuwezesha uwepo
wa Katiba itakayotokana na Wananchi, na hivyo, kuivusha nchi hii kutoka
hapa ilipo na kusonga mbele zaidi.