Dkt. Sengondo Mvungi, akiwa kwenye gari la kubeba wagonjwa, baada ya kufikishwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), akihamishiwa hapo kiutoka Hospitali ya Tumbi, Kibaha Jumapili Novemba 3, 2013.
Dkt. Sengondo Mvungi, amejeruhiwa vibaya sehemu za kichwani na usoni, baada ya kukatwa mapanga, nyumbani kwake, Kibamba Msakuzi, nje kidogo ya jiji, majira ya saa sita usiku Jumamosi Novemba 2, 2013.
Kwa mujibu wa taarifa za ndugu na polisi, Dkt. Mvungi ambaye pia ni Mhadhiri Mwandamizi wa Sheria, Chuo Kikuu cha Bagamoyo, mkoani Pwani, alicharangwa mapanga, baada ya kutaka kujua nini kilichokuwa kikiendelea kufuatia mabishano baina ya mkewe na watu hao ambao walitishia kumuua endapo asingewapa fedha.(P.T)
Taarifa
zinasema, watu hao sita wengine wakiwa nje ya nyumba kwa nia ya kujihami
endapo wangevamiwa na majirani, walivamia nyumba hiyo yenye ghorofa
moja, na kumkuta mkewe Dkt. Mvungi wakati huo Dkt. Mvungi akiwa kwenye
chumba tofauti katika nyumba hiyo.
Kwa
mujibu wa taarifa hizo, wavamizi walipoona mke wa Dkt. Mvungi anachelewa
kutekeleza maagizo yao, walifyatua baruti na hapo Dkt. Mvungi akajaribu
kuelekea kulikotokea mlio huo na ndipo alipokutana na mapanga ya
kichwani na usoni.
Uchunguzi
wa awali wa polisi umeonyesha kuwa tukio hilo ni la kihalifu, kwani
watu hao ambao kwa sasa wanatajwa kama majambazi, waliiba fedha, simu na
laptop, hali inayoonyesha wazi kuwa nia yao ilikuwa ni kutekeleza wizi.
Dk. Mvungi aliwahi kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2005 kwa tiketi ya Chama cha NCCR-Mageuzi.