RAIS KIKWETE ATINGA MKOANI IRINGA TAYARI KUHUDHURIA KILELE CHA MBIO ZA MWENGE



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili Uwanja wa Ndege wa Nduli mjini Iringa leo Oktoba 13, 2013 kuhudhuria Maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwenye wa Uhuru, Wiki ya Vijana na Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere zitaziofabyika kesho (Oktoba 14, 2013) katika uwanja wa Kumbukumbu ya Samora
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na kamnada wa vijana Iringa Mhe Asas katika  Uwanja wa Ndege wa Nduli mjini Iringa leo Oktoba 13, 2013 kuhudhuria Maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwengw wa Uhuru, Wiki ya Vijana na Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere zitazofanyika kesho (Oktoba 14, 2013) katika uwanja wa Kumbukumbu ya Samora.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Iringa mjini Mhe Msigwa katika  Uwanja wa Ndege wa Nduli mjini Iringa leo Oktoba 13, 2013 kuhudhuria Maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru, Wiki ya Vijana na Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere zitaziofabyika kesho (Oktoba 14, 2013) katika uwanja wa Kumbukumbu ya Samora.PICHA NA IKULU.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewasili mjini Iringa jioni ya leo, Jumapili, Oktoba 13, 2013, kwa ziara ya siku mbili ya kikazi mkoani Iringa. Rais Kikwete amefuatana na Mama Salma Kikwete.

                      Shughuli kubwa ambazo Mheshimiwa Rais atazifanya wakati wa ziara hiyo ni kushiriki Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kuwa mgeni rasmi katika Kilele cha Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka huu wa 2013 na Kilele cha Wiki ya Vijana.


Ndege iliyombeba Rais Kikwete ilitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Nduli mjini Iringa kiasi cha saa 12.20 jioni na kulakiwa na umati mkubwa wa wananchi wakiwemo wafuasi wa vyama vya siasa vikiwamo CCM na Chadema.
 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family