Mwanamuziki
Profesor Jay akiwa na mfano wa hundi yenye Barcode ambazo amekabidhiwa
leo, Jay anakuwa mwanamuziki wa Pili Wa Kwanza Akiwa Lady Jay Dee kuchukua Barcode za Tanzania katika
sekta ya muziki wa Bongo Fleva nchini.
Wanamuziki nchini wameaswa kuchangamkia fursa zilizopo kwa
kujitangaza na kutanua wigo wa mashabiki wao kwa kujiunga na huduma ya
Barcode. Hayo yamesemwa leo na mwanamuziki Profesa Jay alipokuwa
akikabidhiwa Barcode za ajili ya CD yake mpya itakayojulikana kama The
Best of Professor Jay ambayo itakuwa na mchanganyiko wa nyimbo zake
ambazo zime heat tangu kuanza kwake. “nimeamua kutoka kivingine na kwa
sasa nataka kufanya vitu kimataifa kwa kusambaza kazi zangu kwenye
mitandao ili niwafikie watu wengi zaidi” alisema Jay.
Akiongea katika makabidhiano hayo Mwenyekiti wa Bodi ya GS1
Tanzania Bw. Elibariki Mmari alisema kuwa ni wakati muafaka kwa
wanamuziki wa Tanzania kuanza kuuza kwenye mitandao ya kijamii na masoko
ya kwenye mtandao kama wanavyofaidi fursa hizo wanamuziki wengine. Bwana
Mmari alisema kuwa kwa kutumia fursa hizo wanamuziki hao wanaweza kuuza
kwenye mitandao ya kijamii kwa kupitia makampuni makubwa duniani kama
CD Baby ambalo lina mikataba na maduka yote makubwa ya kwenye mtandao
kama iTune, Facebook Music na mengine makubwa.
Aidha Mwenyekiti Mmari alitanabaisha kuwa wanamuziki wa Tanzania
hawawezi kuingia kwenye chati kubwa kama za Billboard bila kuwa na
utambulisho wa ki electroniki wa Alama za Mistari yaani Barcode. Naye
Afisa muandamizi wa GS1 Tanzania Bw. Pius Mikongoti alisema kuwa ni
vigumu kupata takwimu sahihi za usambazaji za wanamuziki wa Tanzania
kwani kazi zao haziko kwenye mfumo rasmi, “ukiangalia mwanamuziki kama
Lady Jay Dee mathalani ana wafuasi wamefikia laki moja kwenye mtandao
wake wa kijamii wa Facebook kama atatangaza kuuza kazi zake kwenye
mitandao hiyo ni wazi atawafikia washabiki wake kirahisi zaidi” Takwimu
za Billboard zinachukuliwa kutokana na usambazaji na mauzo ya kazi za
mwanamuziki ki electroniki, ni vigumu kwa mwanamuziki kama Diamond
ambaye kwa sasa ana mashabiki lukuki na kazi zake kupigwa kila kona
kupata takwimu sahihi za usambazaji wake.
Aidha amewataka wadau wa muziki nchini kuacha kusambaza nyimbo
mpya za wanamuziki kwenye mitandao na kuwafanya watu waweze kuzipata
bila kuzitolea chochote (downloads), kwa kufanya hivyo tunawaumiza
wanamuziki na tunakuwa hatuwasaidiii aliongeza Bw. Mikongoti. GS1
Tanzania ndio watoaji pekee wa huduma za BArcode kwa bidhaa zote za
Tanzania, ikumbukwe kuwa ili uweze kuuza kwenye Supermarket na masoko ya
mitandaoni ni lazima uwe na alama hizi za mistari yaani Barcode.
Mwenyekiti
wa Bodi ya GS1 Tanzania Bw. Elibariki Mmari (Mwenye Koti la suti)
akizungumza wakati wa halfa fupi ya kumkabidi Barcode mwanamuziki wa
Kizazi Kipya Profesa Jay katika makao makuu ya Ofisi hiyo TIRDO Msasani
jijini Dar Es Salaam, Kulia kwa Bw. Mmari ni Fatma Kange Saleh Afisa
Mtendaji Mkuu wa GS1 Tanzania na Nd. Pius Mikongoti Afisa Muandamizi
toka GS1 Tanzania na kushoto kwa Mwenyekiti ni Bw. Joseph Haule aka
Profesa Jay.
Mwenyekiti
wa Bodi ya GS1 Tanzania Ndugu Mmari akimkabidi mfano wa hundi yenye
Barcode kwa ajili ya CD na nyimbo za mwanamuziki Pfofesa Jay huku
wajumbe wa Bodi ya GS1 Tanzania wakishuhudia.