Askari
wa Kikosi cha Zimamoto wakitoa elimu kwa baadhi ya wakazi wa Iringa
namna kutumia vifaa vya kuzimia moto na jinsi ya kukabiliana na
majanga ya moto katika maeneo yao leo wakati wa maonesho ya Wiki ya
Vijana Kitaifa yanayofanyika mkoani Iringa.
Baadhi
ya wakazi wa Manispaa ya Iringa waliofika katika banda la maonyesho la
VETA Iringa wakipata maelezo ya bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na na
VETA kutoka kwa Bi. Oliva Adriano mwanafunzi wa mwaka wa 3 katika chuo
cha Ufundi (VETA) mkoa wa Iringa.
Vijana
wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) mkoa wa Iringa wakionyesha ujenzi wa
nyumba za gharama nafuu wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Vijana Kitaifa
mkoani Iringa leo.
Baadhi
ya Watoto wakiangalia banda la Vijana kutoka mkoa wa Dar es salaam na
bidhaa mbalimbali zilizotengenezwa na Vijana hao leo katika viwanja vya
Mlandege mkoani Iringa.
Viunga
vya mji wa Iringa, Mkoa wa Iringa ni Mwenyeji wa Wa Wiki ya Vijana
Kitaifa, kumbukumbu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Kilele cha
Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2013. Picha na Aron Msigwa -MAELEZO.