Wengi tulioangalia movie hii ya
Marekani tumejiuliza wimbo wa Saida Kalori umewafikiaje.Maana ukiangalia
movie hii mwanzoni mwanzoni kabisa wimbo chambua kama karanga unasikika
na anaonekana mama akiucheza kama sehemu ya mazoezi.
Katika movie leo ya leo tena Zamaradi
Mketema aliwahi kuongea na Saida Kalori lakini hakua akijua chochote.Pia
aliyewahi kuwa manager na producer wa Saida hakuwa akijua chochote zaidi
ya kupigiwa simu kutoka Marekani na wanawe walioona hiyo movie.
Sitaki kuisimulia ni movie nzuri ya
kuchekesha...Inamzungumzia kijana anayeenda ukweni kwa mpenzi wake na
anakutana na changamoto nyingi kutoka kwa baba wa msichana na familia
yake kwa ujumla.
Picha zinazopatikana katika movie hiyo.