Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muumgano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akikata utepe kuzindua rasmi Kivuko kipya cha MV Malagalasi kilichopo
Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma, wakati wa hafla ya uzinduzi huo
iliyofanyika siku ya jana wilayani humo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal,
akibonyeza kitufye kuashiria uzinduzi rasmi wa kivuko kipya cha Mv
Malagalasi, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika siku ya jana wilayani
Uvinza Mkoa wa Kigoma. Kulia ni Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe
Magufuli.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,akiwa na baadhi ya viongozi ndani ya Kivuko hicho baada ya kukizindua.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
na viongozi wengine wakitelemka katika kivuko hicho baada ya kukizindua
na kuvuka nacho hadi uapande wa pili.