Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wananchi waliofika
kumpokea kwenye wilaya ya Kishapu katika eneo la Maganzo ambapo Katibu
Mkuu alikuwa na ziara katika wilaya ya Kishapu.
Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupaka rangi moja ya madarasa katika shule ya Sekondari Mwigumbi.
Moja
ya Nyumba mpya iliyojengwa kwa ajili ya makazi ya Walimu wa Shule ya
Sekondari Mwigumbi, wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga ambayo
ilizinduliwa leo na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitumia usafiri wa baiskeli
kufika kijiji cha Mwigumbi ambapo kulikuwa na shughuli za kuzindua
mradi wa maji.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kama ishara ya
kuzindua mradi wa maji wa kata ya Mondo,kijiji cha Mwigumbi wilaya ya
Kishapu mkoa wa Shinyanga.
Mbunge
wa Kishapu Suleiman Masoud Mchambi akishiriki kucheza ngoma ya kiasili
wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji uliofanyiaka kata ya Mondo kijiji
cha Mwigumbi.
Tanki
la maji litakalowasaidia wakazi zaidi ya 4000 katika kijiji cha
Mwigumbi ,pichani wakazi wa kijiji hicho wakiwa wamekusanyika kushuhudia
uzinduzi rasmi wa tanki hilo.
Katibu
Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa
kijiji cha Mwigumbi mara tu baada ya kuzindua mradi wa maji utakaosaidia
zaidi ya watu 4000.
Mbunge
wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Ndugu Azah Hilal Hamad akiwahutubia
wakazi wa kata ya Mondo wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji katika
kijiji cha Mwigumbi.
Mbunge
wa Kishapu Ndugu Suleiman Masoud Mchambiakihutubia wakazi wa kata ya
Mondo na kuelezea namna gani jimbo lake limekuwa mstari wa mbele katika
kutekeleza ilani ya uchaguzi ya chama cha Mapinduzi.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiingia kwenye viwanja vya Mabela
kwa staili ya aina yake tayari kuhutubia wakazi wa Wilaya ya Kishapu.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Balozi wa China hapa
nchini ndugu Lu Youqinq wakati wa mkutano wahadhara uliofanyika katika
viwanja vya Mabela, kushoto kwake ni Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape
Nnauye.