Mrembo
wa Duinia 2013, Megan Young (katikati) wa Philippines akiwa na mshindi
wa pili Marine Lorphelin (kushoto) wa Ufaransa, na mshindi wa tatu
Carranzar Naa Okailey Shooter (kulia) kutoka Ghana.
MREMBO wa Philippines alivishwa taji la binti mzuri zaidi duniani
mwaka huu (2013) jana huko mjini Bali, Indonesia, ambapo kulikuwa na
wasiwasi kwamba Waislam wenye msimamo mkali walikuwa wamedhamiria
kulivuruga tukio hilo.
Mlimbwende huyo, Megan Young, mwenye umri wa miaka 23, aliyezaliwa
Marekani, ambaye anachukua mafunzo ya upigaji wa filamu, alipokea taji
la mashindano hayo kutoka kwa mshindi wa mwaka jana, Wenxia Yu wa China,
na akaahidi kuwa “mlimbwende bora zaidi duniani ambaye hajawahi
kutokea".
Maelfu ya Waislam wa chama cha Islam Defenders Front waliingia
mitaani tangu mwezi uliopita wakipinga kufanyika kwa mashindano hayo
nchini Indonesia, nchi ambayo ina Waislam wengi zaidi duniani, wakiyaita
mashindano hayo kuwa ni “maonyesho ya ngono”.
Upinzani huo uliwalazimisha waandaji kulihamisha tukio hilo kutoka Jakarta kwenda Nusa Dua, kusini mwa Bali.
Katika kulifahamu hilo mapema, balozi za Marekani, Uingereza na Australia zilitoa vibali vya kwenda kwenye shindano hilo kwa kuwaonya wenye kusafiri kwamba tukio hilo la mashindano ya urembo lilikuwa limepangwa kuvurugwa. Hata hivyo, polisi wa Indonesia walisema hapakuwepo na vurugu zozote siku ya Jumamosi.

Marine Lorphelin, mwenye umri wa miaka 20 kutoka Ufaransa, alishika
nafasi ya pili na Carranzar Naa Okailey Shooter (23) kutoka Ghana
alikuwa wa tatu.