CHUO KILICHOVAMIWA NIGERIA HAKIKUA NA ULINZI


    Mauaji ya Nigeria
    Maafisa wa utawala nchini Nigeria wanasema kuwa hapakuwa na ulinzi katika chuo cha mafunzo ya kilimo nchini Nigeria ambako hadi wanafunzi 50 waliuawa Jumapili.
    Wanafunzi waliuawa na watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa kiisilamu katika mabweni yao katika jimbo la Yobe , Kaskzini Mashariki mwa Nigeria.
    Afisaa mmoja alIiambia CHANZO CHA HABARI YETU BBC kuwa serikali itashirikiana na jeshi kuhakikisha kuna ulinzi katika shule.
    Serikali ya Nigeria ilisema kuwa haitafunga shule zingine kutokana na shambulio lililowaua wanafunzi 50 katika chuo kikuu cha mafunzo ya kilimo.
    Shambulio hilo linashukiwa kufanywa na wanamgambo wa Boko Haram siku ya Jumapili.Wavamizi walishambulia kwa risasi chuo hicho kilichoko jimbo la Yobe, kaskazini mashariki mwa Nigeria.
    Afisa mmoja wa serikali Abdullahi Bego, ameambia BBC kuwa serikali na idara ya jeshi zitaongeza usalama katika taasisi zote za elimu.
    Eneo la kaskazini mashariki mwa Nigeria limewekwa katika hali ya hatari kufuatia mashambulio yanayofanywa kila mara na wanamgambo wa kiislamu wa Boko Haram.
    Boko Haram wanadaiwa kupigana kwa lengo la kuiondoa serikali iliyoko na badala yake kuweka utawala wa kiislamu. Tayari wamefanya mashambulio kadhaa katika shule.

    Vyombo vya usalama

    Mwandishi wa BBC wa idhaa ya Hausa, Mansur Liman, anasema kuwa huenda jeshi la Nigeria imelegeza juhudi zake kufuatia kufanikiwa kwao katika siku za hivi punde kuwaondosha wapiganaji wa Boko Haram kutoka maeneo mengi kaskazini mashariki.
    Hata hivyo wapiganaji hao wameripotiwa kuiba sare za kijeshi katika siku kadhaa zilizopita na magari ya kivita. Inadaiwa wanatumia vifaa hivi kupenya maeneo yaliyowekwa ulinzi mkali.
    Mshauri mkuu wa serikali katika Jimbo la Yobe, Abdillahi Bego, ameambia BBC, Jumatatu, kuwa hakukuwepo walinzi katika eneo hilo wakati shambulio lilifanywa katika chuo kikuu.
    Amesema kuwa maafisa wa usalama wa Nigeria walistahili kuimarisha doria katika taasisi za elimu zote.
    Amesisitiza kuwa shule zingine hazitafungwa kwani hilo ndilo hao ''magaidi'' wanataka.
     
    © 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family