MSANII MAARUFU WA FILAMU KUTOKA BONGO AUNT EZEKIEL AFANYIWA UPASUAJI

Kwa mujibu wa mtu wa karibu na staa huyo, Aunt alikuwa akitembea na uvimbe huo siku nyingi pasipo kujijua hadi alipougua ghafla wakiwa katika mizunguko ya kila siku jijini Dar, mwishoni mwa wiki iliyopita. 
“Ghafla alibadilika, hakuwa katika hali ya kawaida kwani tulikuwa tukipiga stori lakini nikashangaa mwenzangu anabadilika kama mtu aliyepandwa na presha hivi.
“Tulilazimika kuahirisha misele yetu, ikabidi twende Hospitali ya Aga Khan na ndipo alipogundulika kuwa ana uvimbe tumboni kisha kufanyiwa upasuaji haraka sana kwani ulikuwa katika hatua mbaya za kuleta madhara,” kilisema chanzo hicho.
Hata hivyo mtu huyo wa karibu ambaye hakupenda jina lake lichorwe gazetini, alisema staa huyo anaendelea vizuri.  
PICHA NA GLOBAL PUBLISHERS
 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family