Mazito yameibuka baada ya msanii mwenye ‘swaga’ za Baba wa Taifa,
Mwalimu Julius Nyerere, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’, kufungua kinywa
na kusema kuwa ugonjwa wake si bure bali amepigwa kipapai.
Akizungumza siku ya Juni 28, mwaka huu, Steve alisema kuwa kufuatia kusumbuliwa na ugonjwa wa ajabu kwa kipindi kirefu sasa na madaktari kushindwa kuelewa kila walipompima, staa huyo anaamini kuwa amerogwa na msanii mwenzake.
“Nimetembea kwa wataalamu wa mambo ya asili na kugundua hilo, sasa ninalazimika kuamini katika imani za kishirikina ingawa ni kitu ambacho muda mrefu nilikuwa nikikipinga sana lakini kwa hili ninaamini kweli nimechezewa na ndiyo maana niko hivi hadi sasa,” alisema Steve bila ya kupepesa macho.
“Nashindwa kumtaja mhusika wa tukio hili kwa sasa ila mwenyewe atakuwa anajua ni kwa kiasi gani nimemgundua, nimejua kwamba wasanii hatupendani hata kidogo na wala hakuna anayependa mafanikio ya mwingine.
“Ipo siku nitamtaja ila leo ngoja niishie kusema kwamba nimechezewa na namshukuru Mungu kwa kuwa hali yangu inaonesha matumaini ya kupona,” alisema Steve Nyerere.
Hivi karibuni, Steve alivimba mkono wake wa kulia, ilifika hatua alishindwa kulala na kutoka nje kutokana na maumivu.