PREZZO NA BIFU LAKE NA DIAMOND

Rapper CMB Prezzo amesema kumuomba Diamond Platnums msamaha kwenye twitter ni utoto na itakua ngumu kwake kufanya hivyo.

Kuanzia 7 July rapper kutoka Kenya Prezzo na mwimbaji Diamond Platnums kutoka Tanzania waliingia kwenye mgongano kutokana na stori zilizoanzia kwenye magazeti.

7 July wote walifanya show kwenye tamasha Uwanja wa Taifa Dar es Salaam ambapo kabla ya hapo kuna interview ambayo iliandikwa gazetini aliyofanyiwa Diamond ambako alikaririwa akisema atamkalisha Prezzo.

Baada ya mgongano kutokea, Diamond alisema hiyo kauli haikua na nia mbaya bali ni kutaka tu kuipamba show lakini anamuheshimu siku zote kama msanii kutoka nyumbani Afrika Mashariki.


Baada ya Prezzo kuiona hiyo message  hakupendezwa hivyo akaingia kwenye kurasa za twitter na kutoa mawazo yake ambayo yalionyesha amekasirishwa kabisa lakini baadae akaagiza timu yake imtafute Diamond ili wayamalize, lakini Diamond akakataa kupokea simu akidai hakua anajisikia vizuri ila akatoa msimamo alioushikilia kwa kumtaka Prezzo akaanze kuomba msamaha kulekule twitter alikoanzia.

Prezzo anasema "maisha huwa hayaendi hivyo, kama Mwanaume mwenzangu ameshaelewa kiini cha hili tatizo lote manake sio nimeamka siku moja nikaamua leo nitamshambulia Diamond, mimi pia namuheshimu ila vitu vingine naona kama kuna utoto unaingilia kati kwa sababu kuomba msamaha kwa twitter, kwa kosa gani? Angepokea simu hii shida isingefika hapa.”



Kwenye line nyingine Prezzo anasema; “mimi sina noma na mtu yeyote licha ya huyo Diamond na najaribu kufanya shughuli zangu kivyangu na naelekea mbele namshukuru Mwenyenzi Mungu, badala ya kuvunja afadhali kujenga... ila kusema ukweli manake mimi ni msema ukweli, hii sijui nimuombe msamaha kwa twitter ni utoto.”

“Roho yangu ni nyeupe, sina damu yoyote mbaya na mchizi tangia zamani hata kabla ya hii Tamasha yeye ni kati ya Wasanii wanaopata heshima kutoka kwangu wakati wowote ule, sina machungu nae... kazi yani iendelee,” asema Prezzo.
 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family