KOCHA
Jose Mourinho amekiri wametoa ofa kwa ajili ya Wayne Rooney na habari
zinasema wamesema wataipa Manchester United hata Pauni Milioni 30
wamnase nyota huyo.
Ndani ya saa 24 tangu vyanzo vya karibu
na Rooney kufichua kwamba ‘ana hasira na amechanganyikiwa’, mshambuliaji
huyo yuko tayari kuwasilisha barua ya kuomba kuondoka, kwa sababu kocha
David Moyes amesema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 hatakuwa
mshambuliaji chaguo la kwanza.
Chelsea ilianza kupeleka ofa ya Pauni Milioni 22 ambayo ilikataliwa na United na sasa wanarudi na ofa iliyonenepa, Pauni Milioni 25— jumla Milioni 3 na inaweza kupanda hadi Milioni 30, ili tu wampate mkali huyo. Ofa ya awali iliyofichuliwa na MailOnline na kukanushwa na Chelsea ilikuwa inahusi fedha na mchezaji kati ya Juan Mata na David Luiz. |
United imekataa ofa ya awali ya Chelsea na kuwaambia wasithubutu kurejea tena, kwa sababu Rooney hauzwi.
Chelsea baadaye ikawatuhumu mabingwa hao wa Ligi Kuu England kwa kuvujisha taarifa za ofa ya awali.
Taarifa kutoka Stamford Bridge
ilisomeka: "Chelsea FC inathibitisha kwamba jana (juzi) imeandika barua
rasmi ya ofa kwa Manchester United kwa ajili ya kumsajili Wayne Rooney.
"Pamoja na hayo, vipengele vya ofa ni
siri, kuepuka shaka na usumbufu uliotokana Mkutano na Waandishi wa
Habari mjini Sydney, mapendekezo ya dau hayahusishi uhamisho wa mkopo au
mchezaji yeyote kutoka Chelsea kwenda Manchester United,".