TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kamati ya Maandalizi ya Mazishi ya Albert Mangweha tunapenda
kuwaatarifu rasmi kuwa mwili wa marehemu Ndugu yetu, mpendwa wetu Albert
Mangweha utawasili kesho tarehe 04/06/2013 saa nane mchana na Shirika
la Ndege la Afrika ya Kusini kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa
Mwalimu Nyerere (Terminal One). Tunaomba mjitokeze kwa wingi kwa ajili ya kumpokea ndugu yetu, mpendwa wetu Albert Mangweha. Taarifa hii kwa mujibu wa Kamati ya Maandalizi ya Mapokezi na Mazishi. Asanteni na Mungu awabariki.
|