BOBANI KUTIMKIA COASTAL UNION

Boban akisaini mkataba wa mwaka mmoja kuichezea Coastal Union.
Boban (kushoto) akiwa ndani ya jezi ya Coastal Union akisalimiana na kocha wa timu hiyo, Hemed Moroko.

Hatimaye aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Haruna Moshi 'Boban' amesajiliwa rasmi na Coastal Union ya jijini Tanga. Boban ambaye hivi karibuni alitangazwa kuachwa na klabu yake ya zamani Simba SC amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuwachezea 'Wagosi wa Kaya'.
Boban aliwahi kuichezea Coastal Union mnamo mwaka 2000 ambapo alidumu hapo kwa mwaka mmoja kabla ya kujiunga na Moro Utd mwaka 2001.

(Chanzo: Shaffih Dauda Blog)


 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family