MWANAMKE ALIYEPIGWA BUSU KWA MARA YA KWANZA NA KUFARIKI PAPO HAPO HUYU HAPA,SOMA MKASA KAMILI


Jemma Benjamini
Kwa mujibu wa mtandao wa telegraph wa Uingereza,
 Msichana  Jemma Benjamini raia wa uingereza ambae alikuwa
 mwanafunzi wa chuo kikuu, alipoteza maisha baada ya kupigwa busu na mwanafunzi mwenzake aliyefahamika kwa jina la Daniel Ross (21) nyumbani kwao na kijana huyo baada ya kutoka kwenye mtoko wa usiku kama marafiki.hiyo ilikuwa ni April 2009
Lakini katika mishemishe za kukaa pamoja
 kwa dakika kadhaa kwenye sofa
 wakibadilishana maelezo kadhaa walijikuta wakikiss taratibu, 
muda mfupi baada ya kiss hiyo Daniel alimuona
 mwenzake analegea taratibu huku macho yake yakiishiwa nguvu na kisha kutulia kabisa.

Hali hiyo ilianza kumtisha kijana huyo ambae anasema 
hawakuwahi kuwa na mahusiano ya mapenzi kabla, na hiyo ilitokea tu wakajikuta wanakiss.
Baada ya hapo alimpigia simu mama yake 
kisha akapiga simu kuomba msaada zaidi wa matibabu 
na ambulance ilifika na kumkimbiza 
hospital ambapo aligundulika kuwa tayari alikuwa ameshafariki. 
Ripoti ya uchunguzi ya daktari ilionesha kuwa 
hakukua na sababu zozote za kimatibabu zilizopelekea kifo chake. Na kwamba kifo cha msichana huyo kimetokana na matatizo 
yanayojulikana kama Sudden Adult Syndrome (SADS), tatizo dogo la moyo linaloaminika kuwauwa watu takribani 500 kila mwaka nchini uingereza.
 
© 2012. Design by Ernest James Siwigo Chambasi - Supported By John James Chambasi And Maganza Family