NEW
UPDATE: Kama wewe unajijua ni msanii wa bongo fleva au Bongo Movie au
kitu chochote na ulikuwa na mapenzi mema na ndugu yetu ALBERT MANGWEHA.
Kuanzia sasa hivi tunatakiwa wote tukutane kule Mbezi Beach kulipo
msiba. Kuna kikao cha watu wotee ili kutoa ratiba kamili na kujua
wangapi watasafiri kuelekea Morogoro kwenye mazishi siku ya Jumanne.
Msiba upo Mbezi Beach kituo kinaitwa Goig ukifika kwenye hicho kituo
utaona boda boda muulizie mtu yoyote ulipo msiba wa Mangweha