Baada ya kumalizika kwa uchunguzi, uliokuwa ukifanyika katika hospitali ya Hillbrow, mwili wa marehemu Albert Mangwea(Pichani) unatarajiwa kuwasili Jumapili kwa ndege ya Shirika la Ndege la Afrika ya kusini, ukitokea nchini Afrika ya kusini. Mwili utapelekwa moja kwa moja katika hospitali ya muhimbili kuhifadhiwa, uletwaji wa mwili huo, ni kwa hisani ya Clouds Media Group. Ndio waliogharimia safari ya mwili wa marehemu. Baada ya Hapo, mwili wa Albert Mangwea utakuwa unaagwa viwanja vya leaders club siku Ya Jumatatu na kampuni itakayoshughulikia zoezi hili ni Entertainment Masters na baada ya mwili kuagwa, safari ya kumsindikiza Albert Mangwea kuelekea kwenye maziko itanza, na hii itakuwa ni kuelekea Morogoro. Mwili wa Mangwea utazikwa Jumatatu katika eneo la Kihonda, mkoani, Morogoro...!! |
Noti mpya kuongia kwenye mzunguko February 1 2025
25 minutes ago